TASAF yasema Jamii nyingi za kitanzania zitaweza kujikwamua na
umasikini kwa kutumia ipasavyo misaada wanayoipata kutoka kwa wahisani
na hata mashirika ya kiserikali na yasiyo ya kiserikali kubuni miradi
mbalimbali itakayowasaidia kukuza vipato vyao.
Ni katika mpango wa TASAF wilayani Monduli mkoani Arusha wa kulipa
kaya masikini katika maeneo mbalimbali nchini ili iweze kuleta tija
katika jamii.
baadhi ya wananchi wa wilaya ya monduli katika kijiji cha mlimani
waliopata fursa ya kupata msaada kutoka Tasaf katika mpango wa
kunusuru kaya masikini wa awamu ya tatu wanasema kuwa msaada huo
utawasaidia katika kuendeleza shughuli mbali mbali za kimaendeleo.
Walengwa ambao ni wananchi wameanza kuekeza kidogo kidogo kwa kutumia
kipato kutoka katika ruzuku ya mpango wa Tasaf wa kunusuru kaya
masikini kama anavyo bainisha mkuu wa mkoa wa Arusha Daudi Ntibenda.
Mfuko wa maendeleo ya jamii Tasaf unalengo la kukuza uwezo kwa
wananchi na kujikimu ususan kwa wale waishio katika hali duni na lengo
ikiwa ni kuwezesha jamii zenye kipato cha chini.
0 comments:
Post a Comment